MCHUNGAJI AASA JAMII KUTUMIA MTANDAO KWA MAENDELEO..........
MCHUNGAJI Hamza Kavenuke wa Kanisa la (EAGT) Kidete, Mufindi mkoani Iringa ametaka matumizi ya wastani ya mtandao ili kuleta maendeleo.
Alisema, vitabu vitakatifu vilikwisha kutabiri kuhusu teknolojia, na kwamba katika hali isiyo ya kawaida, mtandao ulitarajiwa urahisishe maisha sasa unafupisha maisha.
Akizungumza katika ibada ya ndoa, alisema vijana wengi nchini wamekuwa wakipotea kutokana na mitandao na kuwataka wanandoa kutumia mitandao iliyopo kufanyakazi kwa bidii na kujiwekea malengo.
Kwa mujibu wa Mchungaji huyo vijana wanatakiwa kutilia mkazo matumizi bora ya mitandao ili jamii isiendelee kuharibika kimaadili.
Hakuna maoni: