***

***

Technology

Mwanamke alivyokubali mtoto apewe jina la Arsenal.

Shabiki mmoja wa Arsenal alifanikiwa kumshawishi mkewe wampe mtoto wao jina la Arsenal bila mwanamke huyo kugundua hilo.
Ilikuwa ni baada ya miaka miwili ambapo mwanamke huyo Clare Smith alijulishwa ujanja ambao mumewe alikuwa ametumia.
Bi Smith, kutoka eneo la Blacktown jimno la New South Wales nchini Australia, alifichua hayo kwenye barua aliyoandikia jarida moja ambapo anasema mwenyewe hakugundua hilo hadi mumewe alipomwambia.
"Tuliamua kumwita binti wetu Lanesra, kwa sababu lilikuwa jina la kipekee na la kupendeza,” aliandika.
"Ilikuwa ni hadi alipotimiza umri wa miaka miwili ndipo mume wangu akanifichulia kwamba lilikuwa jina la Arsenal ukiandika kutoka nyuma.”
Habari kuhusu kisa hicho zimeenezwa sana mtandaoni, wengi wakijaribu kuandika majina ya klabu za Ligi ya Uingereza kutoka nyuma.
Lanesra (Arsenal)
Retseciel (Leicester)
Yticnam (Man City)
Mahnettot (Tottenham)
Detinunam (Man United)
Mahtsew (West Ham)
Looprevil (Liverpool)
Droftaw (Watford)
Ekots (Stoke)
Notreve (Everton)
Aesnaws (Swansea)
Eltsacwen (Newcastle)
Dnalrednus (Sunderland)
Allivnotsa (Aston Villa)
Aeslehc (Chelsea)
Arsenal kwa sasa wanaongoza katika ligi hiyo ya uingereza.
Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 6 Januari, 2016.
NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Arsenal201642
2Leicester201240
3Man City201839
4Tottenham201836
5Man Utd20733
6West Ham20732
7Crystal Palace20431
8Liverpool20-230
9Watford20329
10Stoke20029
11Everton20727
12West Brom20-526
13Southampton20224
14Chelsea20-323
15Norwich20-923
16Bournemouth20-1221
17Swansea20-919
18Newacastle20-1617
19Sunderland20-1715
20Aston Villa20-218
Reviewed by Unknown on 00:19 Rating: 5

Hakuna maoni:

Gallery

Imetolewa na Alpha Seyongwe. Inaendeshwa na Blogger.