Star wa Soka Tanzania Mbwana Samatta akabidhiwa demu wa kighana....
Binti huyo pamoja na nguli wa televisheni ya SuperSport,
Robert Marawa ndiyo watakaokabidhiwa jina la staa wa Tanzania, Mbwana Samatta
kwenye tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika leo Alhamisi na kumtangaza kama
atashinda tuzo.
Kama ni Mtazamaji Mzuri wa filamu za Ghana na Nigeria utakuwa umewahi kumwona huyu binti anaitwa Juliet Ibrahim. Ana miaka 29 kwa
sasa lakini ni mrembo kinoma. Binti huyo pamoja na nguli wa televisheni ya
SuperSport, Robert Marawa ndiyo watakaokabidhiwa jina la staa wa Tanzania,
Mbwana Samatta kwenye tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika leo Alhamisi na
kumtangaza kama atashinda tuzo.
Juliet
na Marawa watakuwa watangazaji kwenye shoo hiyo ya tuzo za mwanasoka bora wa
Afrika zitakazofanyika mjini Abuja, Nigeria ambayo Watanzania wengi na
mashabiki wa TP Mazembe wanaisubiri kwa hamu.
Mrembo
huyo ambaye ana mashabiki wengi kwenye filamu yuko fiti kwenye lugha ya
Kingereza na baba yake ni Mlebanoni na Mama yake ni Mghana.
Wakuu
wote wa soka duniani wakiongozwa na Alhaji Issa Hayatou wa Fifa
watazishuhudia tuzo hizo.
Katibu
Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameongozana na Samatta anayechezea TP Mazembe
ya Congo DR. Samatta anawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ndani, huku pia akiwa Mfungaji B ora wa michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao manane na
kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo. Samatta anawania tuzo hiyo pamoja na
kipa wa TP Mazembe, Robert Kidiaba na straika wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah
ambaye ni raia wa Algeria.
Reviewed by Unknown
on
01:14
Rating:

Hakuna maoni: