***

***

Technology

Baba mzazi wa Samatta, Mzee Ally Samatta akiwa amepigwa butwaa na ubomoaji wa nyumba ya mwanae.

Baadhi ya watu walidhani ubomoaji huo una uhusiano na operesheni inayoendelea ya Serikali ya Awamu ya Tano ya bomoa bomoa majengo yote yaliyopo mabondeni au katika maeneo yasiyo halali.
 Nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba vinne vya kulala, sebule na vingine viwili vya kulia chakula, jiko na stoo imevunjwa kwa sababu Samatta hajaridhika nayo namna ilivyojengwa na anataka kuporomosha mjengo wenye hadhi yake.
Baba wa straika huyo amefichua kuwa Samatta anataka kujenga ghorofa la kisasa, baada ya usimamizi wa jengo la awali kufanyika ndivyo sivyo na matakwa yake. “Mjengo ulikuwa na nafasi finyu na hivyo anataka kutanua,” anasema. Anasema mbali na ufinyu wa nyumba hiyo, lakini haikuwa na kiwango cha hali ya juu, kwani mvua ikinyesha ilikuwa inavuja, pia ikiwa imetengenezwa kwa vifaa duni tofauti na thamani halisi ya fedha zilizokuwa zikitumwa na mwanaye. 

Reviewed by Unknown on 06:55 Rating: 5

Hakuna maoni:

Gallery

Imetolewa na Alpha Seyongwe. Inaendeshwa na Blogger.