***

***

Technology

WASALIMIE: Benitez atimuliwa Real Madrid


Zinedine Zidane ‘Zizou’  ataiongoza timu kwa hadi mwisho wa msimu, huku akisakwa Kocha mpya ikielezwa Jose Mourinho ana nafasi ya kurudi klabuni hapo, baada ya kutimuliwa Chelsea ya England.

YAMETIMIA. Kocha Rafa Benitez ametemeshwa kibarua chake, baada ya bodi ya klabu ya Real Madrid chini ya Rais Florentino Perez kukutana jana Jumatatu na kufikia maamuzi hayo ya kumtimua kocha huyo.Benitez ametimuliwa ikiwa ni miezi saba tangu ateuliwa kuinoa timu hiyo Juni mwaka jana, ikiwa ni siku moja baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Valencia juzi Jumapili.
Taarifa hizo zimedokeza kuwa nafasi yake imekabidhiwa kwa kiungo wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane ‘Zizou’ ambaye ataiongoza timu kwa hadi mwisho wa msimu, huku akisakwa Kocha mpya ikielezwa Jose Mourinho ana nafasi ya kurudi klabuni hapo, baada ya kutimuliwa Chelsea ya England.
Uvumi wa kutimuliwa kwa Benitez ulianza mapema jioni ya jana baada ya vyombo kadhaa vya habari kudokeza kufanyika kwa kikaohicho na maamuzi yake, ingawa taarifa rasmi iliyoka usiku mwingi kuwa, Benetez ndiyo basi tena Santiago Bernabeu.
Magazeti mawili ya Hispania jana yaliripoti kwamba Zizou anayekinoa kikosi cha akiba cha timu hiyo ndiye aliyekuwa akisubiriwa kutangazwa kushika nafasi ya Benitez aliyeshindwa kupata ushindi katika mechi saba za La Liga. Na katika taarifa hiyo ya usiku wa jana ilithibitisha kuwa ni kweli Zizzou kapewa ‘shavu’ hilo.
Benitez aliyewahi kuzinoa Valencia, Liverpool, Napoli na Chelsea aliyokuwa kocha wa muda, amekuwa katika kipindi kigumu tangu aliporudi Real Madrid kwa mara nyingine baada ya kucheza soka hapo na baadaye kuwa kocha wa timu ya wachezaji wa akiba.
Alirudi kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti, Juni mwaka jana, huku habari za ndani zilidai  baadhi ya mastaa  hawakuufurahia uteuzi wake.
Alijikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya kipigo cha mabao 4-0 ikiwa nyumbani mbele ya Barcelona na hali kuwa mbaya Madrid ilipotolewa kwenye Kombe la Mfalme.
Reviewed by Unknown on 07:10 Rating: 5

Hakuna maoni:

Gallery

Imetolewa na Alpha Seyongwe. Inaendeshwa na Blogger.