***

***

Technology

Magufuli, Lowassa wote kwa Samatta.


Si wanasiasa, si wanamichezo, wasanii na wengine wote walikuwa kitu kimoja wakati walipoungana kutoa salamu za pongezi kwa mshambuliaji nyota wa mpira wa miguu nchini, Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika.

Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa amempongeza mwanasoka wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kwa kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Samatta alichaguliwa jana usiku huko Nigeria kuwa mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza soka barani humu.
Katika pongezi zake, Lowassa ambaye ni mshabiki wa soka asiyependa kuweka wazi anapenda Simba au Yanga, amesema ushindi wa Samatta ni mshabiki wa soka asiyependa kuweka wazi anapenda Simba au Yanga, amesema ushindi wa Samatta ni changamoto kubwa kwa wana soka wa tanzania lakini zaidi kwa Serikali kuwekeza kwenye eneo hilo.
"Huyu kijana kufikia hapo ni kujituma kwake, lakini zaidi ni malezi aliyoyapata katika timu yake ya TP Mazembe...ni lazima tuwe na utaratibu wa kujenga shule za kukuza vipaji vya soka (academy), tutawapata kina Samatta wengi" alisema Lowassa.
Ameongeza kuwa serikali isione shida kuchukua ilani ya CHADEMA iliyoridhiwa na UKAWA ambayo inataka kufutwa kodi kwa vifaa vyote vya michezo.
"Wasione haya kuchukua ilani yetu. sisi tulitangaza kuwa tutafuta ushuru kwa vifaa vyote vya michezo pamoja na kuanzisha Academy ilikuinua vipaji, tunaamini kwa kufanya hivyo watapatikana kina Samatta wengi tu na si katika soka, bali hata michezo mingine kama riadha na ngumi" alisisitiza na kuongeza.
"Kumpongeza tu pekee yake hakutasaidia hawa wengine, ni lazima kuwe na mikakati ya kuwaendeleza vijana wetu hawa. Huwa sipendi kuona wachezaji kutoka nje ndiyo wanaotamba katika timu zetu kubwa, wakati kuna vipaji vingi sana...Kama tukiviendeleza itakuwa kama Brazil au Nigeria..wa nje ndiyo waje kuchukua wachezaji hapa" ameshauri.
Reviewed by Unknown on 00:15 Rating: 5

Hakuna maoni:

Gallery

Imetolewa na Alpha Seyongwe. Inaendeshwa na Blogger.